Mbunge wa jimbo la Ubungo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Saed Kubenea ameunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika ujenzi wa barabara, ukuaji wa uchumi huku akisema anaunga mkono kwa asilimia 200%.

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa barabara ya kilomita 19. 2 unaoanzia Kimara jijini Dar es salaam mpaka Kibaha mkoani Pwani, ambapo amesema uzinduzi huo ni wa kihistoria na wao kama wapinzani wanaunga mkono.

”Kwakweli kwa juhudi hizi mheshimiwa rais Magufuli tunakuunga mkono kwa asilimia 200%, tumeona namna unavyokuza uchumi, sisi tukuhakikishie kuwa tuko pamoja,”amesema Mbunge wa Ubungo Kubenea

Aidha, katika uzinduzi huo wa ujenzi wa barabara hiyo, umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa nchini wakiwemo wa upinzani.

 

Video: Kubenea amfungukia JPM,'Nakuunga mkono kwa asilimia 200%'
Video: Sakata la Membe kitendawili CCM, Vyama 6 vyatoa msimamo mzito

Comments

comments