Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu amewataka wapinzani wake kujenga hoja za msingi na si kueneza propaganda.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa hoja za wapinzani hao kuhusu kujiandikisha Visiwani Zanzibar ni dhaifu na haina mashiko kwani hiyo ndiyo faida ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwamba unaweza ukagombea popote.

“Wanaosema kuwa mimi nimejiandikisha Zanziba wanasema kweli, lakini hoja ya kutokupiga kura mahara fulani hilo haliingiliani hata kidogo, kwani hapa tunaangalia vigezo vya muhusika kama anakubalika na sifa zote zinazihitajika,”amesema Mwalimu

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 9, 2018
Video: Kuondoka kwa mtu ndani ya UKAWA hakuathiri kitu- Salum Mwalimu

Comments

comments