Chama Cha  ACT  Wazalendo kimetoa msimamo wake kuhusu mswaada wa habari  ambao unatarajia kupelekwa Bungeni na kuanza kujadiliwa hivi karibuni  na kuongeza kuwa kama ukipita utakuwa umezika  uhuru wa mawazo, mswaada huu utampa nguvu kubwa Waziri  mwenye dhamana kuzuia uchapishwaji wa habari.

Hayo yamesemwa na Ado Shaibu Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi  makao makuu ya chama hicho yaliyopo jijini Dar es salaam,amesema uzoefu unaonyesha kuwa  madaraka yakiachwa mikononi mwa Waziri  yamekuwa yakitumiwa kuviziba midomo vyombo vya habari.

Amesema kuwa msimamo wa ACT Wazalendo ni kuwa mswaada huo ni hatari kwa uhuru wa wa habari na maendeleo ya demokrasia ya vyama vingi na kuongeza kuwa chama hicho wana ungana na Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya habari (TEF) kupinga uwasilishwaji  bila ushirikishwaji  wadau wa sekta ya habari ili kufanyiwa maboresho.

Aidha, Shaibu amepinga utaratibu wa  utoaji mikopo elimu ya juu ambao amesema  ukiachwa  uendelee watoto wengi kutoka familia masikini watashindwa kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa mikopo.

Video: ACT Wazalendo wapinga utaratibu utoaji mikopo elimu ya juu
Video: Wizara ya ardhi yatoa elimu ya uthamini wa fidia