Chama cha ACT Wazalendo kimepinga vikali utaratibu wa kutoa mikopo unaotumiwa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu, na kusema kuwa kama ukiachwa  mfumo huo uendelee utawafanya watoto wengi kutoka familia masikini washindwe kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa mkopo.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi  Ado Shaibu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  makao makuu ya chama hicho yaliyopo Jijini Dar es salaam, na kuongeza kuwa takwimu zilizotolewa na Bodi ya mikopo kati ya wanafunzi takribani  65000 wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu, ni wanafunzi 20000 pekee waliopata mkopo.

Aidha amesema kuwa hali hiyo ikiachwa iendelee maelfu ya watoto watalazimika kurudi nyumbani kwa kukosa mkopo,na kuongeza kuwa Ilani ya uchaguzi ya ACT Wazalendo ya mwaka 2015 ilipendekeza kuanzishwa  kwa utaratibu wa Scholarship kwa kozi za kipaumbele ili mkopo utumike kusomesha  wanafunzi wengi zaidi.

Shaibu amesema kwenye mikutano ya kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, alisema serikali yake hakutakuwa na mwanafunzi yeyote atakaefaulu  kwenda chuo kikuu, halafu akakosa mkopo, hivyo wamemuomba kutekeleza ahadi hiyo kwa vitendo ya kuwapatia mikopo wanafunzi wa elimu ya juu.

GGM yakabidhi madawati yenye thamani ya mil. 750
Video: ACT Wazalendo wapinga mswada wa habari