Chama cha ACT- Wazalendo kimesema kuwa kinaheshimu maamuzi ya mwanachama wao aliyeamua kujiengua kwenye moja ya nafasi za uongozi huku kikisema kuwa kitatoa rasmi taarifa kwa vyombo vya habari mara baada ya Kamati ya chama hicho kukaa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Ado Shaibu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hii leo, ambapo amesema kuwa wanaheshimu maamuzi ya mwanachama.

“Katika utamaduni wetu wa chama tuliouweka na kuujenga ndani ya miaka mitatu, tumejijenga kwa misingi ya kuheshimiana, hivyo kwa sasa hatutaongea chochote mpaka tutakapo kaa kikao cha chama cha kutoa maamuzi,”amesema Shaibu

Video: Polisi Dar yafanikiwa kuwaua majambazi watatu
Alicho andika Tundu Lissu kwa mara ya kwanza