Chama cha Allience For Democratic Change (ADC) kimesema kuwa kimesikitishwa na kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwafukuza waandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji (TBC) katika mkutano wao uliofanyika makao makuu ya Chadema jijini Dar es salaam.

ADC kimesema kuwa kitendo hicho cha kuwafukuza waandishi si cha kistaarabu wala si uungwana kwani waandishi hao walikuwa katika majukumu yao ya kawaida na ni haki yao kupata habari.

Kimesema kuwa kitendo hicho kilichofanywa na Chadema kuwafukuza waandishi hao kunarudisha nyuma hoja za msingi za kupigania uhuru wa kupata habari ambao ni haki ya kila mtu.

“Tunasikitishwa sana na kitendo kichafu katika ulimwengu wa kistaarabu hasa kipindi hiki ambacho Watanzania wako katika mapambano ya kutafuta uhuru wa habari katika nchi yetu,”amesema Doyo.

Hata hivyo, ADC imewataka Chadema kukaa na kutafakari mustakabali wa Chama chao namna kinavyokimbiwa na wanachama wake, badala ya kujenga uhasama kila kukicha na kada mbalimbali.

Chadema wazishtukia barua za kujiuzulu madiwani wake, 'wameandikiwa'
Tanzania yaombwa msaada na Uturuki