Jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kuhakikisha kijana Saidi Ally aliyefanyiwa kitendo cha kinyama cha kutobolewa macho anaona tena zimegonga mwamba na taarifa za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zimeeleza kuwa aliyemtoboa macho kijana huyo aliharibu baadhi ya mishipa inayompelekea mtu kuona.

Makonda amesema Serikali yake ya Mkoa itamuwekea Said macho ya bandia, kumsomesha, kumpatia fimbo maalum ya walemavu wa macho ikiwa ni pamoja na kumpatia wataalamu maalum kwa ajili ya kumfundisha ili hayazoee mazingira, atapewa dereva maalum ambaye atakuwa anampeleka sehemu mbalimbali ikiwemo hospitali kwa ajili ya huduma tofauti.

Pamoja na hayo yote Makonda amesema Serikali itampatia kiasi cha shilingi milioni 10 ili awekeze kwenye biashara yake ya saluni, na serikali itaandaa kampeni maalum ili aweze kuchangiwa na watanzania wenzake.

Kwa upande wake kijana huyo aliyetobolewa macho Saidi Ally ameeleza kuwa anamshukuru Mkuu wa Mkoa Paul Makonda na Rais Magufuli kwa kuendelea kumuunga mkono, na kueleza masikitiko yake kwakutoweza kuona tena, huku akiiomba Serikali impatie malazi kwanai ni kitu ambacho kinadumu milele. Bofya hapa kutazama video

Video: Kiwanda cha viroba chapigwa faini Shil. mil. 25, chapewa siku 7
Video: Taarifa ya Hospitali kuhusu aliyetobolewa macho na Scorpion