Mbunge wa Iringa Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Msigwa amesema kuwa ziara zinazofanywa na mkuu wa mkoa huo, Ali Hapi ziko nje ya bajeti.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa kitabu cha sera za Chadema.

Amesema kuwa kulikuwepo na wakuu wa mikoa kabla ya Hapi, hivyo wamefanya kazi kubwa zaidi kabla ya mkuu huyo wa mkoa.

“Unajua anachokifanya Ali Hapi ni kitu cha kawaida sana, kuna mifano mingi ya wakuu wa mikoa ambao walishapita na walikuja na mikakati lukuki, kwa mfano Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam yuko wapi sasa hivi, alianza na mikutano lukuki, lakini sasa hivi kimya, Hapi ni maji ya moto atapoa tu na mnamkuza sana,”amesema Msigwa

Hata hivyo, akizungumzia suala la uzinduzi wa kitabu cha sera za Chadema amesema kuwa, kitabu hicho kitakuwa ni muongozo mzuri katika kuliletea maendeleo taifa.

Video: Zitto, Serikali kuliamsha tena, Janga jipya lanyemelea wafiwa wa MV Nyerere
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 2, 2018

Comments

comments