Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba tayari amekabidhi ofisi hiyo kwa Waziri mpya aliyeteuliwa na Rais John Pombe Magufuli, Kangi Lugola leo jijini Dodoma.

Mwigulu ametaja baadhi ya vitu alivyovikabidhi kwa Waziri huyo mpya ikiwa ni pamoja na hotuba ya bajeti ya mwaka huu.

Amesema kwenye hotuba hiyo kuna majukumu ya mwaka mzima yaliyopangiliwa na Serikali pamoja na Wizara kwa mwaka mzima katika mwaka wa fedha 2018/2019.

Ametaja moja ya majukumu hayo kuwa ni pamoja na kuandaa kanuni mpya zitakazo tofautisha bei au faini zitakazokuwa zinatolewa na bodaboda, bajaji pamoja na magari makubwa.

Kanuni hiyo ni kutokana na kuona kwamba madereva wa bajaji na bodaboda wanapata tabu kutokana na kulipa faini sawa na magari makubwa.

Mwigulu amezungumza hayo mara baada ya kukabidhi Wizara hiyo.

Tazama video hapa chini.

Siasa za Ukraine na Urusi zamponza kocha msaidizi Croatia
Picha: Mwigulu Nchemba akikabidhi ofisi kwa Kangi Lugola jijini Dodoma

Comments

comments