Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Oktoba 2, 2016 ametoa taarifa ya Tanzania kupokea wageni mbali mbali kutoka nje akiwemo Makamu wa Rais wa Cuba atakaye wasili leo na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu, Oktoba 3, 2016 Rais Magufuli atampkea Rais wa DRC Congo, Joseph Kabila katika ziara ya siku tatu ndani ya Mkoa wa Dar es salaam, Pia utafanyika mkutano mkuu wa viongozi wa dini ya Mabohora ambapo tayari kuna waumini zaidi ya 300o wameshawasili Dar es salaam.

Makonda amesema kufuatia ugeni huo kutakuwepo faida nyingi kwa wananchi wa mkoa wa Dar es salaam, lakini pia Tanzania kwa ujumla kwa wafanyabiashara, hivyo amewataka Wananchi kuonyesha umoja na kujitokeza kutumia fursa katika ugeni huo. Bofya hapa kutazama video

Orodha ya wadaiwa sugu kutua kwa Waziri Mkuu
Audio: Simba, Yanga zapigwa 'stop' kucheza uwanja wa Taifa