Msanii wa bongo Movie, Wema Isaack Sepetu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametaja changamoto zinazopelekea wasanii wa filamu hapa chini kushindwa kufanya vizuri katika tasnia hiyo.

Wema Sepetu ametaja moja ya changamoto kuwa ni mfumo mbovu wa kuuzia kazi za filamu hapa nchini, kutokana na kuwa na matabaka tofauti kutokana na namna kazi hizo zinavyopatikana kipindi hiki.

Aidha ameiomba Serikali kusaidia katika kutatua changamoto hizo kwani mara nyingi imekuwa ikididimiza kazi za wasanii kwa kuwawekea masharti magumu.

Hayo yamezungumzwa jana katika mkutano ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda uliowahusisha wasanii wa filamu na muziki hapa nchini ambapo walipata nafasi ya kuzungumza changamoto hizo.

Hata hivyo moja ya harakati zilizopangwa ni kuundwa kwa kamati maalumu  ya kupitia changamatoto hizo na kuzitafutia ufumbuzi.

Sikiliza hapa.

Jeshi laapa kuilinda Serikali ya Bashir
Video: Ndugai amlipua Lissu, ambana Zitto

Comments

comments