Msanii wa muziki nchini Alikiba ambaye ametunukiwa ubalozi wa kulitangaza kombe la Dunia linalotarajiwa kurushwa kwa lugha ya Kiswahili katika chaneli ya TBC na TV 1 mwaka huu amewataka watanzani pamoja na wasanii kujivunia kuitwa waswahili na kutumia vyema lugha ya Kiswahili kwa sababu ni lugha kubwa na watu wengi Duniani  hutamani kujifunza lugha ya Kiswahili.

Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuwa watanzania wanapaswa kujivunia kuitwa waswahili na wasione aibu na kuongeza kuwa hata katika nyimbo zake amekua akitumia kiswahili kama kuonesha jitihada za kuunga mkono lugha hiyo.

“Lugha yetu ni nzuri lazima tujivunie, najivunia sana kuwa mswahili na kuongea Kiswahili na kutumia kiswahil katika kazi yangu ya kunipatia maisha, kwahiyo kila mtanzania ni lazima ajivunie kuwa mswahili, asikwambie mtu acha uswahili, ni lazima ujivunie sio sifa mbaya” amesema Alikiba.

Aidha kwa tafiti zilizofanywa zinaoneshwa kuwa kiswahili ni lugha ya kwanza kati ya lugha za asili zinazoongoza kwa kuzungumzwa na watu wengi zaidi, ambapo takwimu zinaonesha kuwa Kiswahili kinazungumzwa na watu zaidi ya Milioni 50.

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Urusi  
Dar24 inakusogeza karibu na Urusi, Kombe la Dunia 2018