Mgunduzi wa wazo la Muonekano Mpya wa Boda boda mkoa wa Dar es salaam, Choba Mumba ameipongeza Serikali kwa usikivu mkubwa kwa vijana na kumpa nafasi ya kufikisha maoni yake hatimaye kufanyiwa kazi.

Mumba amebuni mpango maalumu wa waendesha bodaboda pamoja na bajaji utakaotumika kuwatambulisha sehemu wanazokaa au kupaki.

Katika mahojiano na dar24.com ofisini kwake jijini Dar es salaam, Mbunifu huyo amesema wazo hilo lilikuja kutokana na Madereva wengi wa Boda boda kuvunja sheria mara kwa mara  na kusababisha ajali barabarani  pia usumbufu kwa abiria na wananchi kwa ujumla.

”Hiki ni kitu kikubwa sana kilichonifanya kuanza kufanya utafiti wa  bada boda,nilitaka kujua kwanini jamii inawaona kama wahalifu, kwanini wao ndio wanaoongoza kuvunja sheria za barabarani,kuna kipindi nilitembelea pale hosipitali ya taifa muhimbili na kukuta kuna wodi imetengwa kwaajiri ya boda boda”Alisema Mumba.

Septemba 18, 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amezindua mpango huo maalumu ambapo alisema kuwa utaratibu huo ni maalum kwani sheria itatumika endapo watakaokiuka kutovaa makoti maalumu pamoja na namba ambazo wamepewa watachukuliwa hataua kama hawatatekeleza sheria hiyo.

Makonda aliwataka waendesha bodaboda kuwa mabalozi wa wenzao wanaovunja sheria za barabara kwa kupakiza abiria zaidi ya mmoja. Bofya hapa kutazama video, Mshirikishe na mwingine uwezavyo

Polisi yalegeza Kamba,Yaruhusu mikutano ya ndani ya vyama vya siasa
Andres Iniesta: Niliikataa Ofa Ya Pep Guaradiola