Mkazi wa Chamazi, Omary Chuma anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Pwani, kwa kosa la kutaka kumtapeli mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo baada ya kujifanya ofisa wa Serikali.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ali Mfuru ambapo amesema kuwa Chuma alikamatwa na maofisa wa TAKUKURU, baada ya kupokea taarifa kutoka Kisarawe.

Mfuru ameongeza kuwa, walifanikiwa kumkamata ikiwa ni wiki takribani tatu, zikiwa zimepita tangu wautangazie umma kuhusu, kukamatwa kwa matapali wengine sita walioshirikiana kufanya utapeli.

”Kati ya watuhumiwa hao, wanne walijifanya ni maofisa wa Takukuru wa vyombo vingine vya dola na wawili walitoka katika kampuni ya simu,”amesema Mfuru

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 11, 2019
Balozi wa Uingereza nchini Marekani ajiuzulu