Timu ya Taifa ya Argentina imechezea kichapo cha goli 4-2 dhidi ya Nigeria katika mechi ya kirafiki iliyochezwa nchini Urusi, huku mshambuliaji wake wa kimataifa na Manchester City, Sergio Aguero akidondoka ghafla na kuzimia katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya kumalizika kwa mchezo huo jijini Krasnodar.

Aguero aliifungia timu yake mara mbili kabla ya mshambuliaji wa Nigeria na Klabu ya Arsenal Alex Iwobi kuandika bao la kwanza kwa upande wa Nigeria hivyo kubadili hali ya mchezo huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.

Kelechi Ihenacho aliindikia Nigeria goli la pili kabla ya Ever Banega kuongeza jingine kwa Argentina hivyo kujitwalia ushindi mnono wa magoli manne dhidi ya mawili ya Argentina iliyokuwa ya kwanza kupachika magoli.

Aidha, Aguero alipata fahamu baada ya kukimbizwa hospitali na kupatiwa huduma ya kwanza, hivyo mpaka sasa yuko wodini mpaka pale hali yake itakapoimarika, ingawa mpaka sasa haijajulikana ni kipi kinachomsumbua.

 

Video: Siri ya Masha kujitoa Chadema, 'Bilionea' wa nyumba za Lugumi aelezea alivyotekwa Urusi siku 28
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 15, 2017