Msanii wa nyimbo za bongo fleva, mtaalamu na mwandishi mzuri wa mashairi ya nyimbo zenye mashiko na ushawishi mkubwa kutoka kundi la Yamoto Band lilisosambaratika siku chache zilizopita, Aslay Isihack maarufu kama Dogo Aslay ametoa wimbo mwingine mithili ya taarabu, akiwa amemshirikisha mwanadada chipukizi anayefanya vizuri sana katika tasnia ya bongo fleva na wimbo wake kivuruge, Nandy.

Wamekuja na wimbo mpya ”Subalkheri Mpenzi’ ambapo mpaka sasa unafanya vizuri katika mtandao wa Youtube na umeshika nafasi ya nne kati ya nyimbo zilizopata watazamaji wengi.

Nyimbo hiyo yenye masaa kadhaa tangu ilipoachiwa hewani, mpaka sasa imepata watazamaji 121,737.

Endelea kuipa sapoti nyimbo hiyo kwa Kuitazama, bonyeza link hapo chini.

Kandege avunja mkataba wa TBA na Halmashauri
Aslay amwandikia marehemu mama yake ''Sikufaidika na nilichokifanya kwa miaka 15''