Mkali wa ‘Garagasha’, Azma Mponda ameeleza jinsi alivyoweza kufanikisha kolabo ya kwanza iliyowakutanisha Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi na rapa Izzo Bizness.

Akizungumza hivi karibuni kupitia Burudani24 ya Dar24, rapa huyo aliyewahi kutikisa na albam yake ya ‘Love Story’ amesema kuwa alimtumia wimbo huo Sugu kwa lengo la kutaka kupata maoni yake, lakini mbunge huyo aliupenda na kupendekeza ahusike kwa kuweka madini yake.

Alisema kuwa ‘Garagasha’ ilikuwa imeshafanyika mara mbili awali ikiwa na marapa kadhaa, na iliyokuwepo alikuwa amemshirikisha Wakazi, lakini baada ya Sugu kupendekeza kushiriki kwenye wimbo huo alilazimika kumuondoa Wakazi Swag Bovu aka Bilingual Beast. Hiyo ilipelekea kuwaweka pamoja Sugu, Izzo na yeye ambao wote wanatoka jijini Mbeya.

Msikilize hapa kupata undani, kwanini alimtoa Wakazi, mpango wake wa kuwapa mashabiki zawadi nzito, rekodi ya YouTube Tanzania aliyoivunja, Safari yake ya nchi za nje kama rapa na mengine:

Msongo wa Mawazo kwa Mjamzito Unavyoathiri Akili za Mwanae
Video: Serikali kuboresha maslahi ya wafanyakazi