Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetengua matokeo ya ushindi yaliyompa Ubunge, Onesmo Nangole (CHADEMA)  jimbo la Longid.

Jaji Sivangilwa Mwangesi amesema fomu zilizotumika kuandika matokeo ni fomu za udiwani badala ya kutumia fomu za ubunge hivyo uchaguzi utarudiwa.

Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Longido Dk. Steven Kiruswa.

“Tulikuwa na madai mengi ya msingi lakini moja ni kuwepo kwa kasoro katika utaratibu waliotumia kuhesabu, kujumlisha na kutangaza matokeo ya uchaguzi” – Dk. Steven Kiruswa

Serikali na Kampuni Ya Oracle Waandaa Mkutano Wa Wataalam Wa Tehama
Lionel Messi Aombwa Kutengea Kauli Yake