Wakili wa Kujitegemea kutoka Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume amesema kuwa anatarajia kwenda mahakamani kufungua kesi dhidi ya bao la mkono.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa bao la mkono halikubariki katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika hapa nchini.

Amesema kuwa Wakurugenzi wa Miji na Majiji ndio chanzo kikubwa cha bao la mkono hivyo anakusudia kufungua kesi ya kupinga Wakurugenzi hao kuwa wasimamizi wa chaguzi zinazofanyika kwani wao ni wateule wa rais, hivyo hawawezi kutenda haki kwa vyama vingine.

“Hawa Wakurugenzi ni wateule wa rais, hivyo hawawezi kumuangusha bosi wao, ni lazima watafanya kila wawezalo ili kuhakikisha kuwa bosi wao anapita, sasa hapa ndipo haki ya mpiga kura inapopotea, hawana sifa ya kuwa wasimamizi wa uchaguzi,”amesema Fatma

Hata hivyo, amedai kuwa hata kama akishindwa hatokata tamaa ataendelea na msimamo wake wa kuhakikisha haki ya mpiga kura inapatikana.

Gambo awafunda wanaume, awataka waache Ujuha
Video: Kuna njama za kutupa kesi ya Akwilina - Mbowe, Ajirusha baharini kina kirefu