Usiku wa Oktoba 19, 2016 ni siku ambayo mashabiki wa FC Barcelona wamelala kwa furaha kubwa, pengine hata kukesha kufuatia ushindi mkubwa wa timu yao kutikisa nyavu mara 4 dhidi ya Manchester City katikia mchezo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kabla ya mchezo huo mashabiki wengi wa soka walitarajia Man City kuisumbua FC Barcelona kutokana na Pep Guardiola kuwafahamu, lakini ikawa tofauti kabisa badala yake FC Barcelona ikaibuka na ushindi wa goli 4-0.

Magoli ya FC Barcelona yalifungwa na Lionel Messi (17, 61, 69) na Neymar (89) baada ya kukosa penati dakika ya 87.

Wenger Aweka Hadharani Mchongo Wa Ozil, Alexis
Waamuzi Wa Bongo Wamvuruga Zeben Hernandez