Klabu ya Barcelona imetua nchini Afrika Kusini ambapo inatarajia kushuka dimbani kuchuana na klabu ya Mamelodi Sundowns katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa kwenye uwanja wa FNB stadium.

Mabingwa hao wa ligi ya Hispania wameshuka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oliver Tambo wakiwa na kikosi kamili chenye nyota kama Lionel Messi, Suarez na nyota aliyetangaza kuondoka mwisho wa msimu huu Andres Iniesta.

Barcelona itapambana na klabu ya Mamelodi Sundowns ambao ni mabingwa wa Afrika Kusini kwenye mchezo maalumu kwa ajili ya kumbukumbu ya rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.

Tazama hapa chini Barcelona wakiwasili;

Klabu ya Barcelona imekuwa ikionyesha mapenzi yake kwa kumtambua Nelson Mandela kama mtu wa kipekee katika karne ya 21 aliyekaa jela miaka 27 na badae kuchaguliwa kuwa rais wa Afrika Kusini.

 

Rais John Magufuli akubali kuwakabidhi kombe Simba SC
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Urusi  

Comments

comments