Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limezungumzia hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa vyombo vya usafiri pamoja na sehemu za starehe ambazo zinapiga nyimbo ambazo imezifungia ikiwa ni pamoja na wimbo wa Mwanza/Nyegezi ya Diamond Platinumz.

Akizungumza na Dar24 katika mahojiano maalum yaliyofanyika jana jijini Arusha, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema kuwa Serikali kupitia vyombo vingine itachukua hatua ya kuvifungia vyombo na maeneo husika.

“Mtu yoyote, mahali popote akipiga wimbo ambao umefungiwa… akiweka kwa mfano kwenye vyombo vya usafiri kama basi, vyombo vya usafiri vina mamlaka nyingine ambayo inatoa leseni na leseni ile ina masharti,” alisema Mngereza.

“Au tukiingia kwenye redio  au TV kwa mfano, kuna mamlaka ambayo imetoa leseni kwa ajili ya uendeshaji na leseni ile ina masharti. Kwahiyo ukipiga wimbo wakati Baraza limeufungia maana yake imekiuka masharti ya leseni yako,” aliongeza.


kifafanunua kuhusu kutowafuatilia watu ambao wanaweka kwenye mitandao nyimbo ambazo Baraza hilo limezifungia, Katibu Mtendaji alisema sheria haiwapi mamlaka kwenye matumizi ya mitandao na kwamba hatua zinapaswa kuchukuliwa na taasisi husika, akimaanisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Wanawake wanyoa vipara mbele ya mahakama wakidai waume zao
RC Hapi amkalia kooni aliyemzushia kulazwa makaburini