Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesema kuwa yeye binafsi hamtambui Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Ameyasema hayo wakati akifanya akizungumza katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Cloudstv.

Amesema binafsi hamjui Rais Dkt. Magufuli hivyo hawezi kumhukumu kwa chochote kuwa hashauriki kama baadhi ya wanasiasa wanavyodai.

“Binafsi simjui rais Dkt. Magufuli, kumhukumu kwamba hashauriki nitakuwa nakosea sana, lakini kwa mawaziri waliopo, mwanzoni walikuwa wagumu, lakini kwasasa naona wanabadilika,”amesema Bashe

Video: Mkuu wa mkoa azua kizaa zaa, Mabilioni ya Barrick ngoma nzito
Zuma atakiwa kuchagua moja 'mbivu ama mbichi'

Comments

comments