Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, Hussein Bashe amesema kuwa hakuna tukio baya lililowahi kutokea nchini kama la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha Luninga cha Cloudstv, ambapo amesema ni hatari sana kujenga jamii yenye hofu kwani siku ambayo watu wenye hofu wakiungana nchi haitakalika.

Bashe amesema kuwa watu wamekuwa wakiishi kwa hofu kubwa ya kukamatwa na kutekwa huku vyombo vya dola vipo na havichukui hatua stahiki za kushughulikia tatizo hilo.

Aidha, amesema kuwa wakati umewadia wa kujitazama na kujitathmini kwa Taasisi ya Usalama wa Taifa ambayo imeonekana mfumo wake wa kiutendaji umekuwa ni tishio kwa wananchi.

Heche akerwa na matamshi ya Mnyeti
Mpina awatumbua watumishi 91

Comments

comments