Baraza la vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) wamesema kitendo cha kukamatwa kwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob na kuwekwa mahabusu ni kukiuka sheria.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Patrobas Katambi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 21, 2017 jijini Dar es salaam, amesema “Si kweli kwamba meya alikuwa anafanya siasa alitembelewa na viongozi wengine wa Chadema akawa anawaonyesha mazingira yake ya kazi, ghafla likaja agizo akamatwe, tunaomba tabia hii ikome na safari hii tutachukua hatua,”amesema.

Diamond aachia Video mpya ya 'Fire', itazame hapa
Askari wawili wa usalama barabarani wauawa kwa risasi Kibiti