Mkali wa RnB, Ben Pol ambaye hivi karibuni ameachia audio ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Tatu’ aliyomshirikisha msanii wa Hip Hop, Darassa. Staa huyo ameachia rasmi video ya kazi hiyo ambayo ilikuwa ikisubiriwa na kwamu kubwa sana na mashabiki wake.

Hivi karibuni msanii huyo ‘ali-make headlines’ baada ya kutupia mitandaoni picha zikionyesha yupo nusu utupu akiwa amefungwa kamba, hivyo kwa video aliyoachia ni dhahiri kuwa ametoa majibu ya maswali mengi ambayo yaliibuka kutokana na picha hizo. Tazama hapa video yake. Ukiacha ujumbe wako hapo chini pia utamfikia

Salah ajitia kitanzi Liverpool, aahidi makubwa EPL
JPM ajibu hoja ya wabunge, apiga marufuku wanafunzi wenye mimba