Benki ABC imezindua huduma mpya za uwakala wa huduma za kibenki ikiwa ni moja kati ya mikakati yake ya kuendeleza kuboresha huduma zake na kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora.

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Meneja wa Huduma za Uwakala wa Benki-BANCABC, Mwita Rhobi wakati wa uzinduzi wa huduma hizo, ambapo amesema kuwa lengo la uzinduzi wa huduma hizo ni kutaka kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora.

“Kikubwa kilichotukutanisha hapa leo ni uzinduzi wa huduma hii ya kipekee ambayo itakuwa ni msaada mkubwa sana katika kutoa huduma bora kwa wananchi, kwani lengo letu ni kuwafikia wananchi wote popote walipo,”amesema Rhobi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa huduma za Benki ABC itakuwa na tija kwa Watanzania wote hata wale wasiokuwa na akaunti za benki huduma hiyo itawafikia hivyo kuwa wanufaika wa huduma hiyo.

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 15, 2017
Video: RC Makonda atoa msaada wa miguu bandia