Mfanyabiashara kijana na mwenye mafanikio makubwa nchini, Mohammed Dewji amesema angependa kuwekeza Simba ili kubadili mfumo. Dewji maarufu kama “MO”, amewaambia waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam kwamba bajeti ya Yanga na ile ya Azam FC ni mara mbili ya ile ya Simba, jambo linaloifanya klabu hiyo kuendelea kubaki kuwa msindikizaji. Tayari Mo amesema yuko tayari kutoa Sh bilioni 20 ili kununua hisa asilimia 51 na kuwekeza ndani ya Simba. Tazama hapa video #USIPITWE

Video Mpya: Kazi Kazi - Profesa Jay Ft. Sholo Mwamba
Video: 'Hawatapenya mbele ya Serikali yangu' - Magufuli