Mr Blue alifungua kizibo cha chupa ya maisha yake ya Muziki, Juamapili iliyopita akiwa katika kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm akiongea na mtangazaji wa kipindi hicho, Omary ‘Lil Ommy’ Tambwe.

Blue na Lil Ommy

Blue na Lil Ommy

Katika mahojiano hayo, Blue aliweka wazi jinsi alivyohusika katika kumsaidia Diamond kusambaza wimbo wake ‘Kamwambie’ wakati mwimbaji huyo alipokuwa anasaka tobo la kutokea kimuziki.

Blue ambaye miaka iliyopita aliwahi kuwa kwenye vichwa vya habari akidaiwa kugombea penzi la Wema Sepetu na rafiki yake TID Mnyama, amefunguka ukweli wa yaliyojiri akieleza kuwa ingawa TID alianzisha uhusiano na Wema yeye aliamua kuendelea kuwa rafiki yake kwani binafsi hakuwa na mpango maisha na mrembo huyo.

Muziki ni kitu ambacho msanii huyu ataendelea kukiheshimu siku zote kwani kimemuwezesha kujenga nyumba tatu jijini Dar es Salaam.

Mkali huyo pia amezungumzia jinsi alivyofanikiwa kuachana na uvutaji wa dawa za kulevya aina ya bangi pamoja na mengine.

Angalia hapa:

Video: Hii hapa Helikopta ya Mtanzania Adam iliyozinduliwa
BAVICHA wawajibu UVCCM kuhusu mpango wa kwenda Dodoma