Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limewataka wenyeviti wa mikoa ambayo haijawasilisha majina ya washiriki wa mashindano ya riadha kwa wanawake yajulikananyo kama ‘Ladies First’ kudhibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe  Novemba 22, mwaka huu, mashindano ambayo yatafanyika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Afisa Habari wa BMT, Najaha Bakari alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika mashindano ya riadha.

“Mashindano haya ya riadha yatatoa fursa ya ajira pamoja na kuwakilisha nchi katika mashindao mbalimbali ya kimataifa ikiwemo shindano hili la mwaka 2020 litakalofanyika Tokyo Japan,”amesema Bakari

Amesema kuwa wanatarajia kuwa na wanamichezo 155 katika mbio hizo ambapo kila mkoa utawakilishwa na wanamichezo 4 na kiongozi mmoja.

Aidha, Baraza la Michezo Tanzania limewataka vyama vya riadha ngazi za mikoa kwa kushirikiana na kamati za michezo kuchagua timu zitakazo shiriki katika mashindano ya kitaifa Jijini Dar es salaam  yanayo tarajiwa kufanyika tarehe 24 na 25 Novemba mwaka huu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu msaidiza wa Riadha Tanzania, Ombeni Zavala amewataka vijana kujitokeza katika ushiriki huo kwani ni fursa katika kupata ajira na ameongeza kuwa mikoa inatakiwa kuthibitisha ushiriki wake kwani kuna baadhi ya mikoa imekuwa na tabia ya kutuma majina ya washiriki lakini haishiriki katika mashindano.

Naye balozi wa shirika la JICA nchini, Juma Ikangaa amewaomba Watanzani kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ambayo yanahamasisha vijana wakike katika ushiriki.

 

Takukuru yawashikilia watumishi watano wilaya ya Makete
Jeshi laanza Oparesheni Korosho, lamwaga magari Kusini