Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Gilles B. Muroto amesema kuwa Bodaboda sasa ni janga kubwa kwani kila siku zaidi ya Bodaboda sita wanapoteza maisha kutokana na kutofuata sheria na badala yake wanapakia abiria zaidi ya mmoja (mshikaki) tena bila kofia ngumu.

Kamanda Muroto amesema hayo huko Kigamboni wakati akijibu swali la wananchi katika ziara inayoendelea ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda katika jiji la Dar es salaam.

Amesema kuwa jeshi hilo litaendeleza Operesheni ya kuhakikisha sheria zote zinafuatwa. Tazama hapa

NEMC yaipiga faini ya mil. 15 halmashauri ya Kahama
Walichosema Saut Sol kuhusu bifu la Diamond na Alikiba.