Kufuatia tamko la Serikali la kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu la kutoa siku thelathini kwa wadaiwa sugu waliokopeshwa mikopo na kuchelewa kulipa kwa muda muafaka uliopangwa kurejesha mkopo huo.

Baadhi ya Wadau na Wananchi mbalimbali wametoa maoni yao kwa nyakati tofauti kupitia #SAUTIZETU ya dar24.com kuhusu uamuzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Kati ya maoni hayo ni pamoja na ukukusanyaji wa fedha kwa wananodaiwa ambapo baadhi ya wananchi wamesema kuwa ni mpango mzuri ambao unaweza kusaidia wanafunzi lakini bodi ya mikopo imekurupuka, haijajipanga kwani hata hao wanaowataja wadaiwa sugu na baadhi ya majina waliyoyatangaza siyo ya kweli na wadaiwa hao wamejitokeza hadharani na kukanusha kuwa hawadaiwi na wengine hawajawahi kukopeshwa.

“Bodi ya mikopo ina matatizo sana sababu, wamewataja watu kama Jacobo Steven ambaye ni Meya wa Ubungo, Jerry Muro msemaji wa Yanga, Frederick Mwakalebela na wengine wengi, lakini hawa wote wamekana” amesema mwananchi.

Pia, baadhi ya wananchi hao wameishangaa Bodi hiyo kwamba muda wote huo walikuwa wapi mpaka wanakuja kukurupuka kwa sasa hivi kutoa muda mfupi kama huo

Hata hivyo wameiomba Bodi hiyo kujipapanga kwa kuongeza muda kwa wadaiwa ili waweze kulipa madeni yao vinginevyo hawataweza kufanikisha azima yao.

 

Video: Bodi ya Mikopo yatoa siku 30 kwa wadaiwa sugu

Hakimu awanyooshea kidole Polisi, Magereza kuhusu kesi ya Lema
Super Mario Balotelli Aitamani The Azzurri