Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Esther Bulaya amemjia juu Waziri Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangallah kwa kile alichokidai kuwa kiongozi huyo hakutumia busara wakati akizungumzia suala la sheria mpya ya mifuko ya hifadhi ya jamii mwaka 2018 kupitia mitandao ya kijamii.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi habari, ambapo amedai kuwa kuna viongozi wenzake ambao ni vijana wamekuwa wakimuangusha kwa kuwa wana mamlaka.

“Nimesoma twiti za Kigwangala, mimi nasema yule ni mchumia tumbo anashindwa kutambua kuna wazee wamenifuata kulalamika hawajalipwa mafao kwa miaka 2, anataka tuamini kuwa yale ndiyo maoni ya Baraza la Mawaziri, asisahau hata yeye aliendesha mgomo wa madaktari alivyokuwa Daktari Muhimbili,”amesema Bulaya

Aidha, wakati huo huo Bulaya amemshukuru Spika Job Ndugai kwa kile alichokieleza kuwa amempongeza juu ya msimamo wake kuhusu  suala ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

 

Anthony Joshua awapa Tyson na Wilder wanachokitaka
Sirro afanya mabadiliko madogo ndani ya jeshi la polisi