Mbunge wa Arusha Mjini, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa kwasasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo hakina mashiko tena.

Ameyasema hayo jijini Arusha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa CCM aliyokuwa akipambana nayo kuanzia mwaka 2005 mpaka 2015 kwasasa haipo.

Lema amesema kuwa kwasasa chama hicho kimekuwa kikiwatumia wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi kuweza kuuwa demokrasia kwa kwenda kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi.

Aidha, Amesema kuwa hana uhakika kama uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 mwezi huu kama utakuwa huru na wa haki ambapo amekituhumu chama hicho kuandaa magenge ya wahuni kuvuruga uchaguzi huo.

“Uchaguzi huu wa ngazi ya Jimbo unasimamiwa na Kaimu Mkurugenzi, kwasababu huyu anataka Ukurugenzi, ndio maana wamepanga mikakati ya kuhakikisha wanashinda katika uchaguzi huu,”amesema Lema

 

 

Video: Fredy Lowassa aleta mafuriko Monduli, Unyama wa Polisi kwa Mwandishi wazua taharuki
Manchester United yaanza ligi kwa kwa kishindo, yaweka rekodi lukuki

Comments

comments