Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Fredrick Sumaye amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinalinga kwa sababu kinabebwa na dola hivyo amesema kuwa uchaguzi ujao Chadema itachukua nchi.

Amesema kuwa Chama cha Mapinduzi CCM hakifanyi siasa bali kazi yake kubwa iliyobaki ni kunyofoa madiwani wa vyama vya upinzani huku wakiwa wamejawa na hofu kubwa ya kupoteza nafasi nyingi katika uchaguzi ujao.

“CCM wanakiogopa sana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wanajua kabisa kwamba uchaguzi ujao tutashinda mchana kweupe, hata wananchi wanalijua hilo ila wanaogopa kusema tu,”amesema Sumaye

Hata hivyo, ameongeza kuwa kabla hawajaingia madarakani watafanya kampeni kwaajili ya kuwaeleza wananchi kitu ambacho watakachokifanya pindi tu watakapoingia kuongoza dola.

Watoto pacha walioungana kutenganishwa
Neymar aruhusiwa kufanya mazungumzo na Paris St-Germain