Chama cha Mapinduzi ( CCM) kimesema kuwa kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mke wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kilichotokea jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Hamphrey PolePole wakati wa Ibaada ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa wamepokea kwa masikitiko habari za kifo hicho.

“Tunatoa pole sana kwa Waziri Dkt. Mwakyembe kwa kuondokewa na mke wake, sisi kama umma wa wana CCM tunatoa pole nyingi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, huu ni msiba wetu sote, tuungane na kushikamana,”amesema Pole Pole.

Hata hivyo, Pole Pole amesema Chama cha Mapinduzi CCM, kitamkumbuka Linah Mwakyembe katika mchango wake mkubwa alioutoa katika kukiimarisha chama na kutoa ushauri wa mambo mbalimbali

Bakwata yataka anayejiita Mtume akamatwe
Winnie Mandela aishukia serikali ya Afrika Kusini