Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kuwa kinaridhishwa na utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwakuwa Serikali imejikita zaidi katika kutekeleza Ilani ya Chama hicho ikiwemo kuipeleka Tanzania katika uchumi wa viwanda.

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey PolePole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa CCM imeridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya Tano kwani imefanya ziara ya uhakiki mkoa wa Pwani na kujionea ujenzi wa viwanda vikubwa, vya kati na vidogo.

“Katika kipindi cha miaka miwili cha Uongozi Serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Magufuli, mkoa wa Pwani pekee, umeweza kuwa na viwanda vikubwa, vya kati na vidogo zaidi ya 370, hii ni hatua kubwa sana inayoonyesha kuwa Serikali hii imedhamiria kuifikisha Tanzania katika Uchumi wa Viwanda”, amesema Polepole

Hata hivyo, PolePole amewaasa Watanzania kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda.

Video: Dawa za Kulevya sasa kuwa historia nchini
Video: CCM waunga mkono kauli ya JPM