Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuibuka na ushindi mkubwa katika jimbo la Monduli ambapo mgombea wao Julius Kalanga ametangazwa kupata kura kwa asilimia 95.

Matokeo hayo yametengazwa na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Jimbo la Monduli, Steven Ulaya ambaye ametangaza matokeo ya Jumla ya Ubunge katika jimbo hilo.

Uchaguzi huo ulihusisha jumla ya vyama nane vya siasa vilivyo kuwa vinawania nafasi hiyo ya kupewa ridhaa na wananchi ya kuongoza jimbo hilo hadi mwaka 2020.

Mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Kalanga amewashukuru wananchi wa jimbo la Monduli kwa kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi, na ameahidi kuwafanyia kazi na kuwaletea maendeleo.

Kalanga pia amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumwamini na kumpa nafasi nyingine ya kuwatumikia wanaMonduli kupitia chama hicho.

Arusha kuanzisha mahakama ya jiji, yatenga milioni 20
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 17, 2018

Comments

comments