Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa hama hama ya viongozi inawapa tabu sana wapinzani.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa ndani ya vyama vya upinzani kuna migogoro mikubwa.

Amesema kuwa vyama vya upinzani havina sera ya pamoja ambayo inavitambulisha vyama hivyo kuwa na dira na muelekeo maalumu wa chama.

“Yaani hawa hawana mfumo wa kitaasisi, wanakwenda kienyeji harafu viongozi wao wakihama wanaanza kulaumu, kila mtu ana haki ya kufanya maamuzi,”amesema Polepole

 

Nyota ya Luka Modric yazidi kung'aa
Mnangagwa aahidi kumpa mpinzani wake uongozi