Mbunge wa Jimbo la Siha kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo hakifai kushika dola.

Ameyasema hayo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa alipokuwa mwanachama wa Chadema hakuwa na uhuru wa kufanya chochote.

Amesema kuwa baada ya kukihama chama hicho, wanachama wamemchukia kiasi cha kumpiga ngumi hivyo kitendo hicho kinawashusha hadhi ya kukabidhiwa dola.

“Nilijikuta niko sehemu ambayo kuna watu ambao hawajiwezi, ndio maana nikaamua kuhamia CCM kwenye chama chenye demokrasia ya kweli,”amesema Dkt. Mollel

Aburuzwa mahakamani kwa kumsaidia rafiki yake kujiua
Zawadi 5 muhimu unazoweza kutoa kuelekea siku ya kina baba duniani