Mbunge wa Serengeti Marwa Chacha amefungua kisa kilichomfanya kuhama Chadema na kuhamia CCM, akisema kwamba Chadema ni chama kinachoelekea kuzama.

Akizungumza jijini Dodoma na mwandishi wa Dar 24, Mercy Mbaya amesema kuwa ukiwa kwenye chama cha uipinzani kazi yako kubwa ni kukosoa yale yanayofanywa na chama tawala ili kukipa nafasi chama chako kiweze kushika dola.

Ameongezea kuwa hakuona Chadema ikija kutawala nchi bali ameiona Chadema ikiwa inaelekea ukingoni hivyo aliamua kuruka kwenye mtumbwi huo na kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM.

”Haya maisha wewe binafsi lazima ujiongeze unaangalia mtubwi unazama unasema ngoja niende tu,, ukiona mtumbwi unazama kuna namna ya kuruka unajiokoa , Chadema inazama” Amesema Marwa

Amesema uwepo wa chama cha siasa ni kushika dola na Chadema si chama kinachotarajia kushika Dola, ”nikaona nihame” amesema Marwa.

Video: Makonda ahaidi mamilioni Serengeti Boys wakifuzu michuano ya kombe la dunia
Video: Vijana wanazeeka kwa pombe - Mbunge Kabati

Comments

comments