Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent Mashinji amesema kuwa Chama hicho kinaunga mkono vita dhidi ya kutetea na kulinda rasilimali za nchi lakini kinapinga vita hiyo inavyoendeshwa.

Mashinji amesema dhamira ya Rais Dkt. John Magufuli ya kukabiliana na ufisadi ili ifanikiwe Serikali haina budi kuchukua hatua bila kubagua mtu na cheo chake.

“Viongozi wa serikali ya CCM ndiyo walioshiriki katika kufanikisha kuporwa kwa rasilimali za nchi, Rais Magufuli kama anataka kuchukua hatua basi asibague mtu au cheo cheke,” amesema Dk. Mashinji.

Magazeti ya Tanzania leo Juni 17, 2017
Hamari Traore Apanda Daraja Ufaransa

Comments

comments