Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea amesema kuwa kama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kisingeandamana basi Akwilina asingefariki.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kama Tume ya Uchaguzi ingetimiza majukumu yake, Chadema wasingeandamana na wala pasingetokea kifo.

Aidha, katika hatua nyngine Kubenea amemshangaa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maulid Mtulia kwa kujiuzuru nafasi ya Ubunge ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF) na kujiunga na CCM.

“Kama Tume ingetimiza majukumu yake, Chadema tusingeandamana na wala Akwilina asingefariki, na ninamshangaa sana Mtulia kwa kusahau msaada wangu niliompatia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, Magazeti yangu yalimtangaza na kuandika habari zake bure, lakini leo kasahau yote,”amesema Kubenea

Apokonywa medali Olimpiki ya Pyeongchang
Masoud Djuma: Lazima tuifunge Mbao FC

Comments

comments