Chama cha ADC (Alliance for Democratic Change) kimeeleza kushtushwa na matamko mbali mbali ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yanayohusu kuingilia mgogoro wa Chama cha Wananchi (CUF).

Hayo yamesemwa leo Julai 16, 2017 na Katibu Mkuu wa chama hicho (ADC), Doyo Hassan Doyo wakati akiongeza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kuwa Chadema wamekuwa wakitoa kauli mbali mbali za kuingilia mgogoro unaoendelea CUF mpaka kupanga njama za kibabe kwenda kumuondoa kwa nguvu mwenyekiti halali wa chama hicho.

Doyo amesema Chama chake kinawataka Chadema kuacha mara moja kuingilia mgogoro usiowahusu, kwani kitendo hicho kinaweza kuhatarisha amani ya nchi. Tazama hapa video

Magazeti ya Tanzania leo Julai 17, 2017
Waziri Mkuu Majaliwa akabidhi rambirambi kwa Dkt. Mwakyembe