Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelitaka Jeshi la Polisi na Tume ya Uchaguzi kuwa makini katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Vincent Mashinji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa vitendo ambavyo wamekuwa wakifanyiwa wagombea wao wa udiwani na Ubunge si wa kiungwana.

“Tunapenda kutoa rai kwa vyombo vinavyohusika, Jeshi la Polisi na Tume ya Uchaguzi, vyombo hivi vinatakiwa kuhakikisha watu wao wanasimamia haki,”amesema Dkt. Mashinji

Video: TFDA yaelezea madhara ya kujichubua ngozi
Tanzania yang'ara utawala bora Afrika Mashariki

Comments

comments