Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kuwa amepanga mikakati ya kuwawezesha wachimbaji wadogo wadogo wa madini mkoani humo.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Dar24Media, mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini ulioandaliwa na wizara ya Madini.

Amesema kuwa kupitia mkutano huo wa wadau wa sekta ya madini amejifunza masuala mengi yanayohusu madini na wachimbaji wadogo wadogo.

“Kwakweli niseme ukweli wangu nilikuwa sina uelewa wowote kuhusu madini, lakini kupitia mkutano huu nimejifunza mengi sana, kitu ambacho kimeniwezesha kubuni mikakati ya kuwawezesha wachimbaji wadogo wadogo,”amesema Chalamila

Hata hivyo, mkutano huo wa siku mbili kati ya wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini ulihudhuriwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli

‘Mamilioni ya ‘kubeti’ hatarini kuyeyuka
Video: Majibu sita ya JPM kwa viongozi wa dini, Kortini kwa kumhusisha JPM na sakata la Tril. 1.5

Comments

comments