Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa Chadema si chama cha kigaidi bali ni chama makini.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa chama hicho ni makini na kinapendwa na Watanzania.

Amesema kuwa Chadema iko imara na mbinu zozote za kutaka kukiuwa hazitafanikiwa na kama zikifanikiwa kitakufa chama lakini hisia za watu hazitakufa.

“Mambo haya yanayoendelea kwasasa sio mazuri hata kidogo, kwani kuanza kuzoea kuuawa si kitu izuri hata kidogo bali ni tatizo kubwa,”amesema Mbowe

 

Video: Mtatiro adai kazi ya polisi si kupiga risasi na kuuwa
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 28, 2018