Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhan Madabida amesema  marehemu Mzee Sita alishika nyazifa mbalimbali ndani ya Serikali na chama, amesema kikubwa zaidi ni kuyaishi yale aliyoyapigania na kumuombea kwa mwenyezi mungu ambariki huko aliko.

Mzee Madabida amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo Novemba 7, 2016 nyumbani kwa marehemu Mzee Sita, Masaki Jijini Dar es salaam.

Ameongeza kuwa ndani ya chama ameacha pengo kubwa kwani alipigania kukiimarisha na kukijengea misingi bora, Mzee Madabida ameitaka familia ndugu na jamaa kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki kigumu.aidha pamoja na mengine ameongeza kuwa katika kipindi chake chote alisimamia ukweli na haki na kuongeza kuwa amefanya mengi katika uongozi wake

 

Video: Kifo cha Mzee Sitta ni pigo kubwa sana kwa wanamsasani – Mangula

Video: Simba tumepata pigo kubwa sana - Rage
Video Mpya: Rayvanny - Sugu