Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya bongo Fleva Said Juma ‘Chege’ amewapa zawadi mashabiki wake kwa kuachia wimbo mpya anaokwenda kwa jina la Njegeka ambao amemshiriksha nyota mwenzie Vanessa Mdee.

Kwa mujibu wa Chege, kibao hicho ambacho tayari kina video yake, ameamua kumshirikisha Mdee ili kuleta ladha hasa kwa kuzingatia kuwa ni mwnadada mwenye kipaji cha hali ya juu katika muziki wa kizazi kipya.

“Nimekuwa nikitamani kufanya kazi na vanessa Mdee zaidi ya miaka mitatu iliyopita lakini sasa nimefanikiwa kumshirikisha kwenye wimbo wangu mpya, Vanessa ni msanii wa kipekee na tofauti kutokana na kujitoa kwake kwenye ngoma pale anaposhirikishwa, kushauri na hata kuongeza baadhi ya viunjo na kufanya kazi ikapendwa” amesema Chege.

Na kuongeza kuwa Njegeka maana yake ni mapenzi yasiyoeleweka yani ya kudanganya hivyo mashabiki wa muziki wake wataona ngoma hiyo ilivyo ya kitofauti na upekee.

Pia amesema kwa upande wake mitandao ya kijamii ni sehemu kubwa ya kufahamiana na mashabiki wake kwani amekuwa akijifunza mengi na kujua mashabiki wake wanahitaji nini kutoka kwake.

RC Chalamila awataka viongozi kuacha unafiki
Halmashauri zaombwa kujifunza ujenzi wa soko la Njombe

Comments

comments