Bondia Maarufu nchini Tanzania, Francis Cheka amefunguka na kusema kuwa ameshawahi kutuhumiwa kutumia nguvu za giza katika mapambano yake ya mchezo wa ngumi.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24Media, ambapo amesema kuwa tuhuma hizo si za kweli bali ni watu wenye nia mbaya ndio wanaosambaza uzushi huo.

Amesema kuwa siri ya mafanikio ni kujituma na kwamba amekanusha tuhuma hizo za kujihusisha na nguvu za giza katika mapambano yake ya mchezo wa ngumi,

“Kwakweli tuhuma za uchawi katika maisha yangu ya mchezo wa ngumi si za kweli, watu wamekuwa wakisambaza uzushi huo kwa nia ya kuniharibia maisha yangu, mimi namiliki biashara mbalimbali, hivyo wanataka kuharibu ili nikose wadhamini wa kuniwezesha kupiga hatua mbele katika maisha yangu,”amesema Cheka

Aidha, Cheka ameishauri serikali kuajiri vijana katika nyanja mbalimbali za michezo ili kuweza kuwa na idadi kubwa ya wanamichezo nchini.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kuna vijana wengi ambao amesaidia katika mchezo huo wa masumbwi nchini, kitu ambacho amewataka vijana hao  kujiheshimu na kufanyakazi kwa bidii.

 

Video: Cheka afunguka kuhusu uchawi, 'mimi sijihusishi na nguvu za giza'
Matokeo kidato cha nne: Necta yataja shule 10 zilizofaulu zaidi, mwanafunzi bora

Comments

comments